Israel imethibitisha kumuua kiongozi mpya wa Hamas

Muhammad Sinwar aliuawa katika shambulio la anga kusini mwa Ukanda wa Gaza mwezi uliopita, kwa mujibu wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF).

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limethibitisha rasmi kuuawa kwa kiongozi wa Hamas, Muhammad Sinwar, katika shambulio la anga lililofanyika mapema mwezi huu katika mji wa Khan Younis ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa taarifa ya IDF iliyotolewa Jumamosi, shambulio hilo lilitekelezwa Mei 13 kwa ushirikiano na idara ya usalama ya Shin Bet. Jeshi hilo limesema kuwa shambulio hilo lililengwa katika kituo cha chini ya ardhi cha uongozi kilichokuwa kikitumiwa na Hamas chini ya Hospitali ya Ulaya.

"Tumemuua Kiongozi wa Hamas, tena. Kwa bahati mbaya naye ni Sinwar," IDF iliandika katika mtandao wa X.

Sinwar alichukua uongozi wa Hamas baada ya IDF kumuua kaka yake, Yahya Sinwar, pamoja na kamanda mwandamizi Muhammad Deif mwezi Oktoba.

Magaidi waliuawa wakiwa ndani ya kituo cha uongozi na usimamizi kilichokuwa chini ya ardhi, chini ya Hospitali ya Ulaya huko Khan Younis, wakiweka makusudi hatarini maisha ya raia walioko hospitalini na maeneo ya jirani," IDF ilisema.

IDF imesema kuwa Sinwar alikuwa na "jukumu kubwa katika kupanga na kutekeleza mauaji ya kikatili ya Oktoba 7."

Tangazo hilo limetolewa wakati pande zote mbili zikidaiwa kuonyesha nia ya kukubali pendekezo la usitishaji mapigano lililosimamiwa na Marekani.

Katika operesheni hiyo pia waliuawa Muhammad Shabana, kamanda wa Brigedi ya Rafah ya Hamas, na Mehdi Kuwara, mkuu wa kikosi cha Khan Younis cha kundi hilo. IDF iliwatambua wote wawili kuwa ni washirika muhimu waliopanga mashambulizi ya Oktoba 7 na utekaji wa mateka wa Kizayuni.

Hamas haijathibitisha wala kukanusha taarifa ya kifo cha Sinwar. Kundi hilo la wanamgambo hapo awali lilikana tuhuma kwamba linatumia miundombinu ya kiraia kujificha. Maafisa wa afya wa Gaza walisema wakati huo kuwa watu 28 waliuawa katika shambulio la Mei 13.

Shambulio hilo liliripotiwa wakati ambapo Israel ilikuwa imeongeza mashambulizi yake Gaza, kufuatia kuvunjika kwa makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyosimamiwa kimataifa mwezi Machi.

Ingawa ripoti zinaonyesha kuwa Israel na Hamas wamekubaliana kwa kauli juu ya muundo mpya wa usitishaji mapigano, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesisitiza kuwa operesheni za kijeshi zitaendelea hadi Hamas itakapoteketezwa kabisa. Baada ya shambulio la hospitali, aliahidi "kuingia kwa nguvu kamili kukamilisha operesheni na kuwaokoa mateka waliobaki."





Comments