EU imesitisha mali na kuwekeza vikwazo dhidi ya kundi la waasi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) la Syria kwa tuhuma za kuwaua watu.

Muungano wa nchi za Ulaya (EU) umeweka vikwazo dhidi ya jeshi la Syria linaloongozwa na kundi la waasi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), kwa kushiriki katika mauaji ya raia wa jamii ya Alawite kando ya pwani ya nchi hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.

EU imeweka vikwazo kwa vikosi vitatu: Sultan Suleiman Shah Brigade, Hamza Division, na Sultan Murad Division, kwa tuhuma za kulenga raia, hasa jamii ya Alawite, kwa njia ya mauaji ya kiholela na ukatili mwingine wa haki za binadamu.

Viongozi wa vikosi hivyo, Mohammad Hussein al-Jasim na Sayf Boulad Abu Bakr, wamewekewa marufuku ya kuingia EU na mali zao zimezuiliwa.

HTS iliteka mji wa Damascus Desemba 8, 2024, ikimaliza utawala wa miaka 24 wa Assad, na tangu wakati huo imehusika katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, hasa dhidi ya makundi madogo kama Alawite na Druze.

Mzozo wa kidini unaendelea, kama ilivyoonyeshwa na mapigano kati ya HTS na jamii ya Druze, ambayo hapo awali ilikuwa na uungwaji mkono wa serikali ya Assad.

Kwa upande mwingine, muungano wa kampuni za Marekani na baadhi ya makampuni ya kikanda umeingia mkataba wa dola bilioni 7 na utawala wa HTS kuhusu nishati, lengo likiwa kuzalisha megawati 5,000 kwa kutumia teknolojia ya Marekani na Ulaya.

Mkataba huo ulisainiwa Damascus na kuhudhuriwa na kiongozi wa HTS, Abu Mohammed al-Jolani, na balozi wa Marekani Thomas Barrack.

Mabadiliko haya yanakuja baada ya HTS kuchukua madaraka, na kupelekea upungufu mkubwa wa mafuta kutoka Iran na kukwama kwa huduma za umeme nchini Syria.

Jolani, aliyewahi kuwa na uhusiano na al-Qaeda na Daesh, aliongoza waasi wa HTS kuangusha serikali ya Rais Bashar al-Assad mwaka jana.

Baada ya kuchukua madaraka Desemba, HTS na Jolani walianza juhudi za kujaribu kuondoa mjadala kuhusu historia yao, ikiwemo kuanzisha mawasiliano rasmi na mataifa ya Magharibi kama Ufaransa.

Matukio haya mapya yanajiri huku Marekani ikiwaelekeza watawala wapya wa HTS Damascus kuanzisha uhusiano na Israel.

Trump alitangaza kuwa ataondoa vikwazo vyote vya Washington dhidi ya Syria baada ya serikali mpya katika nchi hiyo ya Kiarabu kuripotiwa kupendekeza kufanya “amani” na utawala wa Israeli, mshirika wa karibu wa Marekani katika eneo.

Trump alionyesha baada ya kukutana na Jolani wakati wa ziara yake katika baadhi ya mataifa ya Ghuba ya Uajemi kwamba kiongozi wa Syria alikuwa tayari hatimaye kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel.

Rais huyo pia alitoa ishara kwa utawala wa Israeli kwamba unapaswa kufanya juhudi za kufikia makubaliano na viongozi wa HTS.

Kwa upande mwingine, Israel pia imekuwa ikihamasisha Washington kuendelea kuweka Syria dhaifu na isiyo na utawala wa kati.

Israel na Syria wako katika mawasiliano ya moja kwa moja na wiki chache zilizopita wamefanya mikutano ya uso kwa uso baada ya al-Jolani wa Syria kuonyesha hamu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Israeli.


Comments